Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee Na Watoto Dkt. Godwin Mollel ameupongeza uongozi wa Wilaya ya Ileje Mkoa wa Songwe kwa kusimamia vyema fedha za ujenzi wa hospitali ya wilaya kwa kujenga majengo ambayo thamani ya fedha inaonekana.
Dkt Mollel amesema hayo alipokwenda wilayani humo kukagua hatua za ujenzi wa hospitali hiyo ambapo Serikali imetoa kiasi cha tsh bilioni 1.8 kwa ajili ya ujenzi.